Arusha Forum
Headlines News :

ad300x250

Total Pageviews

Ads 468x60px

Featured Posts

Footer Widget 1

Footer Widget 2

Social Icons

Latest Post

RC aonya NGOs, vigogo wa wilaya ya Ngorongoro

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, June 3, 2013 | 11:50 AM

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo


MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali (NGOs) na Baraza la wafugaji wilayani Ngorongoro wameonywa kuacha kunogewa na fedha haramu wanazozipata, zinazowatuma kuchochea vurugu baina ya wananchi, mamlaka ya hifadhi na serikali.

Mbali ya NGOs, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wanaotaka kuwania ubunge wa Jimbo la Ngorongoro mwaka 2015 na mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Saning’o ole Telele na Mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Mathew ole Timani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Ngorisa, wametakiwa kuacha kutumia mgogoro huo kujitafutia umaarufu.

Onyo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara baina yake wananchi na viongozi wa kata ya Enduleni wilayani Ngorongoro ili kutatua mgogoro kati ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na wananchi walio ndani ya hifadhi hiyo.


Mulongo alisema mashirika hayo na wanasiasa hao, wamekuwa wakiwapotosha wananchi kuwa serikali imewatelekeza.

Alisema serikali ina mpango wa kuiingiza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, iwe chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wananchi hao watalazimika kufukuzwa.

Alisema kwa muda mrefu, asasi hizo na wanasiasa wamekuwa wakichochea vurugu kwa kutoa matamshi yasiyo ya kiungwana, ikiwemo kuhakikisha wanafanikiwa malengo yao ya matumizi ya fedha walizopewa na wafadhili wao pasipo kuangalia athari za matamshi yao kwa nchi.

Mulongo alisema hivi karibuni mashirika, asasi na baraza hilo la wafugaji, wamefikia hatua ambayo si nzuri ya kuwasemea wananchi hadi kutoa matamko ambayo ni hatari.

Pia, walitoa masharti kuwa iwapo serikali itaendelea kushikilia uamuzi wake wa kuwaondoa wananchi hao katika maeneo yao, watashirikiana nao kufunga mageti ya kuingilia watalii ndani ya hifadhi hiyo ili kuzuia shughuli za utalii.

Hata hivyo, alilinyoshea kidole baraza la wafugaji Ngorongoro kwa kuwawezesha chini kwa chini wananchi na baadhi ya viongozi wa serikali na madiwani kwa mambo mbalimbali ya kichochezi, ikiwemo gharama za kwenda mikoa ya Dodoma,Dar es Salaam na hata mjini Arusha kwa ajili ya kuendeleza vurugu hizo.

Akiwazungumzia wanasiasa hao, alisema wamekuwa wakichuana katika kampeni zao zisizo rasmi kwa kutumia mgogoro huo usio na mantiki, kujitafutia umaarufu.

Alitaka watumie njia nyingine ya kutafuta umaarufu huo badala ya kuendelea kuwagawa wananchi na hifadhi na serikali yao.

By John Mhala, Arusha

Mh. Lowassa aipongeza kampeni ya hoteli ya Double Tree kwa kutoa taa za nishati ya jua

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Friday, May 31, 2013 | 1:19 PM

Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann akifafanua jambo kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa (kulia) ambapo amemweleza kuwa huu ni mwendelezo wa Kampeni yao itakayodumu kwa takribani miaka miwili tangu walipoanza na lengo likiwa nikuwafanya wanafunzi hususani wa darasa la saba wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao katika hafla fupi iliyofanyika ofisini kwa Mh. Edward Lowassa jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoulbeTree by Hilton Florenso Kirambata.

Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (katikati) akimkabidhi moja kati ya taa 200 zinazotumia nishati ya jua Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoulbeTree by Hilton Florenso Kirambata akishuhudia tukio hilo kwenye hafla fupi iliyofanyika Ofisini kwa Mh. Edward Lowassa jijini Dar.

Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoulbeTree by Hilton Florenso Kirambata akikabidhi baadhi ya taa zinazotumia nishati ya jua kwa Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Monduli Jumanne Masuke. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa ( wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (wa pili kushoto).

Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa akitoa shukrani kwa uongozi wa DoubleTree Foundation ambapo ametumia fursa hiyo kuitaka serikali kuwekeza sana katika elimu ili kuweza kukuza uchumi.Aidha amesema ni vyema kuwekeza katika sekta ya elimu ili tuweze kusonga mbele na kuwa na kizazi cha watu wenye elimu kwani masikini asiye na elimu ni hatari kuliko mtu yeyote, kwa kuwa mtu anapopata elimu anakuwa na ufahamu unaomuwezesha kukabiliana na maisha ya kila siku.



Picha juu na chini ni Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (katikati) na Kushoto ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoulbeTree by Hilton Florenso Kirambata mara baada ya kukabidhiwa taa 200 zinazotumia nishati ya jua atakazozigawa katika jimbo lake kwa shule za msingi.

Blogger Themes

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger