VIONGOZI NA WANACHAMA 15 WA CHADEMA KUTIMKIA NCCR MAGEUZI LEO - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » VIONGOZI NA WANACHAMA 15 WA CHADEMA KUTIMKIA NCCR MAGEUZI LEO

VIONGOZI NA WANACHAMA 15 WA CHADEMA KUTIMKIA NCCR MAGEUZI LEO

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Saturday, February 2, 2013 | 9:23 PM

 

VIONGOZI waandamizi wa Chama Cha Demokrasia

na Mendeleo CHADEMA pamoja na wanachama 15 wa chama

hicho wanatarajia  kujiunga na Chama Cha NCCR Mageuzi leo katika  ukumbi wa

Hotel ya Double J jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa taarifa za chama hicho zilizotumwa kwa  njia ya ujumbe

mfupi wa simu ya mkononi kwa wanahabari imedaiwa

kuwa viongozi  hao wa CHADEMA watakutana na Mjumbe wa

 Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi na mshauri wa mambo ya kisiasa Danda

 Juju ambaye atamwakilisha, mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho

 James Mbatia.Juju ambaye tayari amewasili mkoani Mbeya kwa

shughuli hiyo  maalum anatarajia kuwapokea viongozi hao wa CHADEMA

ikiwa ni hatua  za awali zinazodaiwa kukisambaratisha CHADEMA.

Hivi karibuni aliyewahi kuwa Katibu wa Mkoa wa

CHADEMA Eddo Makata alitangaza kujiunga na NCCR-Mageuzi

baada ya kujiuzulu kutoka

CHADEMA ambapo hata hivyo viongozi wa CHADEMA

walidai kuwa walimtimua uongozi na uanachama.
Wimbi la mpasuko ndani ya CHADEMA limeanza kuibuka

baada ya madai ya kutimuliwa kwa viongozi na wanachama wa chama

 hicho akiwemo, Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana la

Chadema Taifa (BAVICHA)Juliana Shonza na aliyewahi kugombea

Ubunge jimbo la Mbozi Mashariki Mtera Mwampamba
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger