Waliotaka kuiba kwa January Makamba watiwa mbaroni - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Waliotaka kuiba kwa January Makamba watiwa mbaroni

Waliotaka kuiba kwa January Makamba watiwa mbaroni

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Sunday, February 10, 2013 | 11:38 PM

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January  Makamba.
POLISI Mkoa wa Kipolisi  Kinondoni, linawashikilia watu kadhaa  kwa tuhuma za ujambazi walioufanya katika nyumba ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January  Makamba  Februari 3 mwaka huu. Ujambazi huo ulifanywa wakati naibu waziri huyo akiwa safarini jimboni kwake  Bumbuli huku nyumbani hapo ikiwepo familia yake ambapo mlinzi alifungwa kamba na kuzibwa mdomo na majamazi hao.

Katika tukio hilo majambazi hao hawakukamilisha azima yao kwa kuwa mke wa naibu waziri huyo alibonyeza kengele ya tahadhari mapema ambayo ilipiga kelele zilizowaogopesha majambazi hao ambao walikimbia ili kujiokoa na kukamatwa. Baada ya tukio hilo,Kamanda  wa Polisi Kinondoni, Charles Kenyela  aliahidi kuwasaka na kuwakamata watu waliohusika.

Na Julius Mathia
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger