Mkutano wa CCM wavurugwa kwa mawe - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Mkutano wa CCM wavurugwa kwa mawe

Mkutano wa CCM wavurugwa kwa mawe

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Friday, February 8, 2013 | 2:46 AM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo 
Kwa ufupi
Akiwa na baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali, Bulembo aliwasili katika viwanja hivyo saa 11:00 baada ya kuketi ndipo mawe yalianza kurushwa kutoka nje ya uwanja kuelekea

 KUNDI linalodaiwa kuwa la wafuasi wa Chadema juzi lilivamia Mkutano wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo na kufanya vurugu ambazo zilisababisha watu kadhaa kujeruhiwa.

Vurugu hizo zilitokea kwenye mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya mwenyekiti huyo katika Mji wa Mlandizi, Mkoa wa Pwani.

Mwenyekiti huyo ambaye hivi sasa yuko ziarani mkoani Pwani juzi alipangiwa azungumze na wakazi wa mji huo juu ya masuala mbalimbali, lakini muda mfupi alipowasili uwanjani hapo mambo yalibadilika ghafla na kuanza kwa vurugu hali iliyosababisha kutoweka kwa amani katika eneo hilo .

Akiwa na baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali, Bulembo aliwasili katika viwanja hivyo saa 11:00 baada ya kuketi ndipo mawe yalianza kurushwa kutoka nje ya uwanja kuelekea maeneo walikokuwa wameketi wanachama wa CCM pamoja na watu wengine

Hali hiyo ilidumu kwa takriba ni saa moja huku baadhi ya wanachama wa pande mbili wakionekana wakiwa katika mvutano na kurushiana makonde na kugombea bendera ambapo wa upande wa Chadema walikuwa wakipora bendera za CCM jambo lililowafanya nao wa CCM waanze kupora bendera za Chadema.

Katika kipindi chote hicho mwenyekiti huyo alionekana akiwa ameketi pamoja na baadhi ya viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa huku wanachama wa pande mbili wakiendelea na mvutano mkali ambapo watu watatu walijeruhiwa na kupelekwa katika Kituo cha Afya Mlandizi na baadaye kupelekwa Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya matibabu.

Baada ya hali ya vurugu kupungua katika eneo hilo ndipo viongozi mbalimbali wa (CCM) walianza kupanda jukwaani tayari kwa kuanza kuzungumza huku wakiwatupia lawana polisi kwa kile walichoeleza kuwa hawakuwajibika ipasavyo katika kutuliza vurugu hizo.

“Napenda kusema kuwa watuwaliotufanyia fujo wapo mpaka sasa hapa uwanjani na tumesha watambua kwa majina na mahali wanapoishi na tutahakikisha wanakamatwa na sheria inachukua mkondo wake,” alisema.

Aidha ilidaiwa kuwa katika vurugu hizo jenereta lililokuwa likitumika kwenye mkutano huo kama chanzo cah umeme lilipotea katika mazingira ya kutatanisha pamoja na bendera za wanachama wa CCM.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger