MFANYABIASHARA AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA WA BINADMU ILOLO MBEYA - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » MFANYABIASHARA AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA WA BINADMU ILOLO MBEYA

MFANYABIASHARA AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA WA BINADMU ILOLO MBEYA

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Wednesday, February 13, 2013 | 11:13 AM


BARAKA KIBONA, MIAKA 30,MNDALI,MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILOLO AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU HAPA AKIWA NDANI YA GARI YA POLISI
 
MTUHUMIWA AKIPAKIWA NDANI YA GARI YA POLISI
 
HAYA MABOKSI INNASADIKIWA YALITAKIWA YAJAE HELA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA
 

 BAADHI YA WANANCHI WA MTAA WA ILOLO WAKISHANGAA TUKIO HILO NYUMBANI ALIKOPANGA MTUHUMIWA HUYO


 MNAMO TAREHE 12.02.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO ENEO LA ILOLO JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WALIMKAMATA BARAKA S/O KIBONA,MIAKA 30,MNDALI,MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILOLO AKIWA NA KIUNGO CHA BINADAMU SEHEMU YA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA NDANI YA NYUMBA YAKE.

MBINU ILIYOTUMIKA NI KUFICHA KIUNGO HICHO CHUMBANI NDANI YA BOX KWA KUZUNGUSHIWA KAMBA . MTUHUMIWA ANAKIRI KUMILIKI KIUNGO HICHO AMBACHO ANADAI ALIPEWA NA MGANGA WAKE WA KIENYEJI KWA MADHUMUNI YA KUKITUMIA KIUNGO HICHO KWA AJILI YA KUJIKINGA/KUJILINDA KATIKA BIASHARA ZAKE ZA KIMACHINGA ZISICHUKULIWE KWA NJIA YA KISHIRIKINA IKIWA NI PAMOJA 
NA FEDHA ZAKE.

 TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO JAMII KUACHA TABIA YA KUSADIKI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WAFANYE KAZI ZAO KWA BIDII KWA KUMCHA MWENYEZI MUNGU KUPITIA IMANI ZA DINI ZAO.

 AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUENDELEA KUUCHUKIA UHALIFU KWA KUWAFICHUA WAHALIFU NA UHALIFU KATIKA MAMLAKA HUSIKA UNAOJITOKEZA KATIKA MAENEO YAO.
 Signed by

[B.N.MASAKI -SSP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MBEYA
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger