HOYCE TEMU ATUA IRINGA, AJICHANGANYA NA WADAU - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » HOYCE TEMU ATUA IRINGA, AJICHANGANYA NA WADAU

HOYCE TEMU ATUA IRINGA, AJICHANGANYA NA WADAU

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Saturday, February 9, 2013 | 11:25 AM

Hoyce Temu akimsikiliza kwa makini Rais  wa serikali ya  wanafunzi  chuo  cha Tumaini Iringa
Hoyce  Temu akipozi kwa  picha na mzee wa matukio  daima  Francis Godwin baada ya  kufanya mahojiano juu ya ziara  yake mkoani Iringa
Hoyce Temu alipojichanganya vidanda  vya UVCCM na  kukutana na wana, mwanahabari  wa Chanel Ten Clement Sanga , Afande Bashiri  na mwanahabari Denis Mlowe
Wadau   wakifurahi kuwa na mrembo Hoyce Temu

Miss Tanzania wa mwaka 1999   Hoyce  Temu ametua mkoani  Iringa na  kujichanganya na  wananchi  wakazi  wa mkoa  wa Iringa katika maeneo ambayo si rahisi  kwa  star kama  huyo  kujichanganya .

Temu alishangaza  wengi na kuonekana ni mtu  wa watu baada ya  kuacha kujirusha  katika maeneo maarufu na  kulazimika  kujichanganya  na  wana Iringa katika  Grosari  za  vibanda  vya UVCCM mjini Iringa na  kuwapa ofa ya  kinywaji wadau waliofika kumsabai kwa  salamu.

Hata  hivyo Temu ambae yupo mkoani Iringa  kwa ajili ya kuandaa  kipindi chake  cha  MIMI NA  TANZANIA  kinachorushwa  katika  kituo cha Chanel Ten amesema kuwa lengo lake ni  kuendelea kuheshimu taji lake kwa  kufanya mambo mazuri katika jamii badala ya  kujivunjia  heshima  yake .

Amesema  kuwa atapenda  kuona watanzania  wanaendelea kumpongeza kwa kazi zake badala ya kuendelea  kumdharau  ,hivyo amesema  ataendelea  kufanya makubwa katika Taifa.

Kwa  upande  wake  wakazi  wa mkoa  wa Iringa  walimpongeza mrembo  huyo  kwa kazi nzuri anazozifanya katika jamii na kuwa katika maisha yake hapaswi kuiga mambo ya  warembo wengine ambao  wameshindwa kujiheshimu na kuonekana ni wachafu  wa  kutupwa katika jamii  kutokana na kuwa na skendo kila  kukicha.

Bila  kuwataja majina  ya  warembo hao walisema  kuwa picha ya kuwa urembo ni uhuni  imekuwa  ikichafuliwa na warembo  wanaoshika nafasi kama  hizo na  mara  baada ya kuwa maarufu wanaanza  kuutumia umaarufu  huo  kuuza miili  yao.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger