Washerehekea kifo cha Waziri Mkuu Uingereza - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Washerehekea kifo cha Waziri Mkuu Uingereza

Washerehekea kifo cha Waziri Mkuu Uingereza

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, April 11, 2013 | 3:20 AM

 Waandamanaji wa Uingereza wakiwa waameumia kichwani baada polisi kuwatandika kutokana na kusherehekea kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Magret Thatcher.  

Wakati Waingereza wengi wakihuzunika kwa kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Magreth Thatcher, kundi moja la wakazi wa nchi hiyo waliamua kuandamana huku wakinywa pombe na kufurahia kicho cha kiongozi huyo.

Watu hao walionyesha kufurahia kifo cha mama huyo ambaye alikuwa waziri wa kwanza wa kike nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya kimataifa, mamia ya wakazi katika Miji ya Brixton na London Kusini walionekana wakiwa na michoro mbalimbali ya kumkashifu marehemu.

Sababu za kuandamana hazikuwa wazi, lakini wengi wanaamini kwamba ni kutokana na msimamo mkali wa marehemu Thatcher.

Kwa nyakati tofauti wakazi wa miji hiyo walioneka kusherehekea kifo hicho kwa kunywa pombe na kuchora picha zenye mionekano ya ajabu,

huku wakiliandika jina la Waziri Mkuu huyo wa zamani kwenye mabango yao ambayo walikuwa wakiyatembeza.

Polisi katika maeneo hayo wanawashikilia baadhi ya watu waliokuwa kwenye makundi wakishangilia na kunywa pombe tangu saa 11.0 jioni ya juzi.

Zaidi ya watu 300, vijana na wazee walisherehekea hadi wakati wa usiku katika Mitaa ya London, wakiwa na makopo ya maziwa mikononi huku wakicheza muziki wa rege.

Watoto wadogo walionekana wakiambatana na wazazi wao, huku wengi wakivalia nguo na nywele za bandia .
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger