RIDHIWAN KIKWETE ATANGAZA ORODHA YA WAJUMBE TISA - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » RIDHIWAN KIKWETE ATANGAZA ORODHA YA WAJUMBE TISA

RIDHIWAN KIKWETE ATANGAZA ORODHA YA WAJUMBE TISA

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, April 15, 2013 | 11:12 AM



 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYdeAd02xYclKuPP13oQmSEur9fGr6M2tSpmU0zjXZ0MQ4cUmyrE5M6_y6evW1fSkBGTlaRJO5qFV546apGjmqxLIXwc8uf1OnZlpRtqm9wrfNStoT2vkdaX12GHJkdp8le-y3E99m8dcV/s1600/dd34ba7dd1L.jpg

Mwenyekiti wa kamati hiyo Ridhiwan Kikwete ambaye ametangaza leo orodha ya wajumbe tisa atakaosaidiana nao katika kuhakikisha wanajenga jengo hilo lililopo mtaa wa Mafia na Nyamwezi wakiwemo NAIBU Waziri wa Miundo Mbinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Issa Haji Usi na Jaji 

Mstaafu Jaji John Mkwawa watakao ongoza kamati ya ujenzi wa jengo la Yanga lililopo mtaa wa Mafia.

Kikwete Jr.alisema kuwa Naibu Waziri huyo wa Zanzibar ndio atakayekuwa Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo akisaidiana na Jaji John Mkwawa.

Alisema wajumbe wengine ni Baraka Ingangula ambaye ni mtaalamu wa majengo na kwamba atasaidia kuwapa mchoro wa kujenga jengo la kisasa lenye hadhi na imara.

"Inabidi tutafute mtu ambaye atatusaidia katika usanifu wa jengo tukalojenga hatuwezi kujijengea tu siku mbili limeanguka kama mengine yanavyoanguka na kutuletea shida."alisema Kikwete Jr.

Mbali na Igangula pia amemteua Allan Magoma kutoka Tanzania Investment Bank, Charles Palapala (mfanyakazi wa benki), Izack Chanje (Injinia) na wakili Mavalle Msemo.

Kikwete Jr.alisema kuwa mbali na wajumbe hao pia ameunda kamati ndogo ambayo itakuwa na jukumu la kufatilia masuala mbali mbali ya ujenzi wa jengo hilo ambayo itaongozwa na Katibu wa Yanga Laurance Mwalusako akisaidiwa na Beda Tindwa na Mohamed Milando.

Kikwete Jr. alisema kuwa wiki ijayo anatarajia kukutana na kamati yake na kupeana majukumu ikiwa ni pamoja na kupokea michoro mbali mbali ya majengo ambayo wataiangalia na kujua thamani alisi ya jengo ambalo watalijenga.

“Tumeshawapa notisi wapangaji wa jengo hilo ili watupishe tuanze ukarabati haraka iwezekanavyo. Tunataka tuwe na jengo la kisasa ambalo litakuwa na manufaa kwa klabu kwa kuhakikisha linakuza uchumi wa timu.

“Naahidi kujenga ghorofa kubwa lenye hadhi, ndio maana nimeteua wajumbe wenye uelewa mkubwa nitakaosaidiana nao,” alisema Ridhiwani Kikwete.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger