Mwenyekiti wa kamati hiyo Ridhiwan Kikwete ambaye ametangaza
leo orodha ya wajumbe tisa atakaosaidiana nao katika kuhakikisha wanajenga
jengo hilo lililopo mtaa wa Mafia na Nyamwezi wakiwemo NAIBU Waziri wa Miundo
Mbinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Issa Haji Usi na Jaji
Mstaafu Jaji
John Mkwawa watakao ongoza kamati ya ujenzi wa jengo la Yanga lililopo mtaa wa
Mafia.
Kikwete Jr.alisema kuwa Naibu Waziri huyo wa Zanzibar ndio
atakayekuwa Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo akisaidiana na Jaji John Mkwawa.
Alisema wajumbe wengine ni Baraka Ingangula ambaye ni
mtaalamu wa majengo na kwamba atasaidia kuwapa mchoro wa kujenga jengo la
kisasa lenye hadhi na imara.
"Inabidi tutafute mtu ambaye atatusaidia katika usanifu
wa jengo tukalojenga hatuwezi kujijengea tu siku mbili limeanguka kama mengine
yanavyoanguka na kutuletea shida."alisema Kikwete Jr.
Mbali na Igangula pia amemteua Allan Magoma kutoka Tanzania
Investment Bank, Charles Palapala (mfanyakazi wa benki), Izack Chanje (Injinia)
na wakili Mavalle Msemo.
Kikwete Jr.alisema kuwa mbali na wajumbe hao pia ameunda
kamati ndogo ambayo itakuwa na jukumu la kufatilia masuala mbali mbali ya
ujenzi wa jengo hilo ambayo itaongozwa na Katibu wa Yanga Laurance Mwalusako
akisaidiwa na Beda Tindwa na Mohamed Milando.
Kikwete Jr. alisema kuwa wiki ijayo anatarajia kukutana na
kamati yake na kupeana majukumu ikiwa ni pamoja na kupokea michoro mbali mbali
ya majengo ambayo wataiangalia na kujua thamani alisi ya jengo ambalo
watalijenga.
“Tumeshawapa notisi wapangaji wa jengo hilo ili watupishe tuanze
ukarabati haraka iwezekanavyo. Tunataka tuwe na jengo la kisasa ambalo litakuwa
na manufaa kwa klabu kwa kuhakikisha linakuza uchumi wa timu.
“Naahidi kujenga ghorofa kubwa lenye hadhi, ndio maana
nimeteua wajumbe wenye uelewa mkubwa nitakaosaidiana nao,” alisema Ridhiwani
Kikwete.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !