Dar es Salaam
MAKAMU Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) Juliana Shonza pamoja na baadhi ya wanachama wengine akiwemo Mtela Mwampamba, na Habib Mchange wamefukuzwa uanachama katika chama hicho huku wengine wakisimamishwa uongozi na wengine kupewa onyo kali.
Hatua hii imetafsiriwa kuwa ni msimamo wa Dk Slaa pamoja na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ambao wameelezwa kuwa wanakisafisha chama kwa lengo la kuingia ikulu kwa kishindo mwaka 2015.
Kabla ya kutimuliwa Mwampamba aliwahi kugombea ubunge kupitia chadema katika jimbo la Mbozi wakati Mchange aligombea ubunge jimbo la Kibaha lakini kura hazikutosha.
Aliye pewa karipio kali ni Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Mbeya Mr Kasambala wakati Gwakisa anayetokea Wilayani Rungwe akisimamishwa uongozi wake.
Fuatana nasi kwa ajili ya habari zaidi

0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !