Sehemu ya watuhumiwa wa vurugu za Mtwara wakikamatwa mmoja baada mwingine. |
Hali ya utulivu inadaiwa kurejea katika Wilaya ya Masasi mjini Mtwara baada ya vikosi vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Polisi kuungana kuweka ulinzi huku watu zaidi ya 40 wakiwa wamekamatwa kuhusika na matukio ya vurugu za jana.
Kutokana na vurugu hizo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi wako Mtwara wakiendelea na vikao vya kurejesha amani na utulivu mkoani hapo.
Pia inadaiwa mida ya asubuhi Jumapili,27,2013 jana palilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya vijana ambao walikuwa wamefunga barabara na kuwatoza ushuru batili wa Shilingi 5,000/= wenye magari kama sehemu ya kujipatia fedha kwa njia feki.
Aidha shughuli za ibada ziliendelea kwa utulivu zaidi.
Aidha vijana hao walivamia nyumba ya Anna Abdalah na kuiteketeza kwa moto, kabla ya kuivamia ofisi ya CCM Wilaya na kuichoma moto pamoja na magari matatu inasemekana wamekwisha teketeza nyumba ya Mbunge wa Masasi (Mama Kasembe), Vifaa vya Mahakama ya Mwanzo pamoja na magari ya Halmashauri,Ofisi ya Elimu ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Vijini kabla ya kuchoma moto Ofisi ya Mali ya Asili.
Maandamano hayo yanasemekana yaliongozwa na Madereva wa bodaboda.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !