Jeshi la Wananachi JWTZ kwa kushirikiana na polisi limefanikiwa kumkamata kijana aliyejidai kuwa ni mwanajeshi wa jeshi hilo kikosi cha Monduli.
Kijana huyo alipiga picha na Mbunge wa Arusha Godbless lema alipokuwa akiwasalimia wananchi baada ya kurudishiwa ubunge wake na mahakama ya Rufani kitendo ambacho ni kosa kwa Mwanajeshi yeyote nchini kushabikia habari za vyama.
Aidha uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini kuwa Kijana huyo hakuwa mwanajeshi wa JWTZ kama alivyojitambulisha kwa viongozi wa Chadema na kwa waandishi wa habari bali aliwahi kuwa JKT na akaacha.
Uchunguzi huo pia umebaini kuwa Kijana huyo alikuwa akivaa nguo hizo za Kijeshi mara kwa mara kwa miaka mingi hivyo mkuwafanya wananchi wa Mererani kumtambua kuwa mwanajeshi.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !