Mwandishi wetu Robert Hokororo
Na Baltazar Mashaka, MWANZA
Na Baltazar Mashaka, MWANZA
SERIKALI imeonya kuwa nchi inaweza kugawanyika vipande viwili kwa sababu Wakristo wanataka kuchinja kama wanavyofanya Waislamu.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira maarufu kama Tyson muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa kutafuta suluhu ya kuchinja kati ya Waislamu na Wakristo.
Alisema suala la Wakristo kutaka kuchinja halina msingi wowote kwa vile nia ya Serikali ni kuona biashara hiyo inakuwa ya jamii yote, hivyo litabaki kuwa chini ya Waislamu, ingawa hoja hiyo ilipingwa na Wakristo.
Wassira alidai kuwa suala hilo limeleta mvurugano usio na sababu, hivyo Serikali inahitaji uchinjaji wanyama kwa ajili ya kuuza uwe unaofaa na kuonya vita zinazopiganwa katika mataifa mbalimbali zinaongozwa na viongozi wa dini.
Kwa sababu hiyo alipendekeza kuundwa kwa chmbo cha kuunganisha madhehebu hayo. Wassira alisema chombo hicho kitakuwa cha kumzungumzia misuguano baina ya dini hizo chini ya mfumo watakaojiwekea viongozi wenyewe.
Kuhusu suala la Wakristo kutaka kuchinja ambalo limezua mvurugano ndani ya jamii, alisema hilo litaendelea kubaki kwa Waislamu kwa ajili ya kuuza na kuomba jamii isikwazike kwa hilo.
”Kuwa na mabucha ya Wakristo na Waislamu tutaanzia hapo kugawanyika na tutakuwa na misingi ya kuigawa nchi vipande viwili. Na yapo mambo ambayo lazima tuvumiliane, haiwezekani yote yakakubaliwa.
“Kwa biashara hilo litabaki hivyo, sababu mambo ya kuchinja hayana msingi na Serikali inataka biashara iwe ya jamii yote,” alisema Wassira. Aliwaambia vongozi wa Waislamu na Wakristo kuwa nchi ni yetu sote, hivyo tusichezee amani iliyopo.
”Ninyi viongozi wa kidini mnatulea, ukienda kanisani au mskitini wote unaona ni wafuasi wako wote… kumbe wamo Chadema na CCM, lakini wao hawasemi mimi ni CCM au Chadema kwa vile mnadhamana hiyo mtusaidie kuhubiri amani ili hao wanaohubiri fujo wakose njia. Kwani waumini wenu wanavunja sheria, hawataki utii wa sheria bila shuruti hivyo tofauti zao za kisiasa ziwe za amani,” alisema.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti mara baada ya kumalizika kwa mkutano bana yao na Waziri, viongozi hao walisema hawapo tayari kushiriki kwenye chombo hicho hadi watakapoelezwa madhumuni yake ni yapi.
Kuhusu suala la Wakristo kutaka kuchinja ambalo lilikuwa agenda kuu ya mkutano huo wa siku mbili ulifanyika ukumbi wa Halmashauri ya Jji la Mwanza, walidai kuwa limeamuliwa kisiasa ili kuwabeba Waislamu.
Askofu Agustine Mpemba wa Kanisa la Tanzania Field Evangelism (TFE), alisema uamuzi uliotolewa na Wassira ni wa kisiasa huku akilalamika kuwa zama hizi ambazo maarifa yameongezeka haiwezekani wakaendelea kuburuzwa na kunyimwa haki.
Wakati Wakristo wakikataa mapendekezo ya Serikali, Waislamu kupitia kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Quran na Sunna Tanzania (Jaqusuta), Shekhe Hassan Kebeke, alisema kimsingi wao wameridhika.
”Wakristo wana nafasi yao ya kufanya hivyo kwenye familia, mtu akikualika wewe Mwislamu anakufanyia heshima, hatakufanyia kinyume cha utaratibu.
”Hivyo tunawajibika kuwaelimisha waumini wetu kuwa Mkristo asizuiliwe kuchinja kwa mahitaji ya familia yake,” alisema Sheikh Kebeke.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !