Kwa ufupi
“Ninazo sababu zilizonisukuma nifanye uamuzi huu
mgumu tena wenye maumivu makali kwangu kadri ninavyofikiri nilivyojitoa
kuijenga Chadema kwani chama kinatambua mchango wangu, lakini siwezi
tena kuendelea kufanya kazi na watu wasioniamini na wenye kasi ya
kunichonganisha na umma”alisema. CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) Mkoa wa Mbeya kimepata pigo baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa kujiuzulu uanachama wa chama hicho.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari jana mjini hapa, Edo Mwamala alisema kuwa ameamua kuchukua uwamuzi huo kutokana na hoja ya kuambiwa amehongwa mamilioni ya fedha na CCM.
“Ninazo sababu zilizonisukuma nifanye uamuzi huu mgumu tena wenye maumivu makali kwangu kadri ninavyofikiri nilivyojitoa kuijenga Chadema kwani chama kinatambua mchango wangu, lakini siwezi tena kuendelea kufanya kazi na watu wasioniamini na wenye kasi ya kunichonganisha na umma”alisema.
Alieleza sababu nyingine kuwa ni pamoja na suala la Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbroad Slaa kuwa na kadi ya CCM “sikubaliani na suala hili nataka airudishe ama awajibike kisiasa na mgawanyo wa rasilimali za chama ni utata mtupu,mkoa kama Mbeya wenye Chadema ya kweli haujapewa hata kipaza sauti wakati magari yote na vifaa vyote vimehodhiwa makao makuu, huu ni zaidi ya ufisadi tunaopigia kelele”alisema.
Alisema kuwa chama hicho kimekuwa na migogoro isiyo na suluhu wa mlingano katika kuitatua mfano ni Mwanza na Arusha ambapo Chadema imewafukuza madiwani lakini Karatu nyumbani kwa Slaa wanabembembelezwa “hapa pana ajenda ya kuifanya Chadema iwe ni Saccos tu ya wajanja wachache”alisema.
Mwamalala alisema kuwa kumekuwepo na maandamano ya kudai haki na kufanyika katika mikoa ya Mwanza,Arusha na Mbeya ambako viongozi wake wakiongea ukweli wanafukuzwa,lakini hata siku moja haijaitishwa Moshi na Karatu ili nako Wananchi wa kule waonje joto ya jiwe ya kupambana na polisi.
“Kuna hoja ambazo tumeendelea kuzilea ndani ya Chadema na hatimaye zimezaa ulemavu wa demokrasia ya kibabe mfano suala la ukanda kuwa na nguvu kaskazini lina nafasi yake”alisema.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !