Messi awa mwanasoka bora kwa mara ya nne - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Messi awa mwanasoka bora kwa mara ya nne

Messi awa mwanasoka bora kwa mara ya nne

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Wednesday, January 9, 2013 | 7:37 PM

Lionel Messi



MWANASOKA wa Argentina, Lionel Messi aliibuka kidedea baada ya kutangazwa Mwanasoka Bora wa Dunia kwa mwaka 2012 jana ....

Messi anakuwa mwanasoka wa kwanza kushinda tuzo hiyo kwa mara ya nne mfululizo.

Messi aliibuka kidedea baada ya kuwashinda Andres Iniesta na Cristiano Ronaldo.

Muargentina huyo alikuwa anastahili tuzo huyo kutokana na mambo makubwa aliyofanya mwaka jana.

Messi alizamisha mabao 91 na kuisambaratisha rekodi ya Mjerumani Gerd Mueller kwa kufunga mabao mengi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Alipachika mabao hayo katika mechi alizochezea Barcelona na timu ya taifa ya Argentina.

Mueller aliweka rekodi yake mwaka 1974 wakati alipofunga mabao 85 wakati akiwa katika timu zake za Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani.

Messi alikabidhiwa tuzo yake na Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia na beki wa zamani wa Italia, Fabio Cannavaro na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Pia katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na magwiji wa sasa na wale wa zamani wa soka, Messi alitajwa katika Kikosi Bora cha Dunia cha mwaka 2012.

Kikosi hicho kilikuwa kimesheheni nyota wa timu pinzani za Hispania za Barcelona na Real Madrid. Mmoja tu ndiye alitoka timu tofauti.

Iker Casillas wa Real Madrid ndiye aliyetajwa kama kipa wa kikosi wakati mabeki bora walikuwa David Alves (Barcelona), Gerrard Pique (Barcelona), Sergio Ramos(Real Madrid) na Marcelo (Real Madrid)

Wachezaji wa kiungo walikuwa Xabi Alonso (Real Madrid), Xavi Hernandez (Barcelona) na Iniesta (Barcelona.

Messi ndiye aliyeongoza safu ya ushambuliaji akiwa na Ronaldo (Real Madrid) na Radamel Falcao (Atletico Madrid).

Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka ilikwenda kwa Vicente Del Bosque baada ya kazi nzuri ya kuiongoza Hispania kutwaa taji la Euro 2012.

Staa wa Fenerbahce ya Uturuki, Miroslav Stoch aliibuka kidedea kwa kufunga bao bora na tuzo hiyo alikabidhiwa na nyota wa zamani wa Colombia, Carlos Valderrama. Aliwashinda Neymar wa Brazil na Falcao.

Abby Wambach wa Marekani naye alitangazwa kuwa Mwanasoka Bora kwa upande wa wanawake. Wambach anasifika kutokana na mashuti yake makali kwenye safu ya ushambuliaji.

Naye Kocha wa Marekani, Pia Sundaghe alipata tuzo kama kocha bora wa timu ya wanawake.

Naye Blatter alitoa tuzo yake maalumu kwa staa wa zamani wa soka wa Ujerumani, Franz Beckenbauer kwa mafanikio yake makubwa katika soka.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger