Kenyatta, Uhuru waifunika Kenya - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Kenyatta, Uhuru waifunika Kenya

Kenyatta, Uhuru waifunika Kenya

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Saturday, January 12, 2013 | 10:30 PM

Kwa ufupi
Wanasiasa hao walianza kufanya mkutano huo mjini Mombasa ambao  baada ya hapo waliendelea na mkutano wao katika mji wa Nakuru huku wakiwa na idadi kubwa ya wafuasi.

 WANASIASA maarufu nchini Kenya  Uhuru Kenyyata na Williamu Ruto, wamefanya mkutano mkubwa mara baada ya kuungana rasmi.

Wanasiasa hao walianza kufanya mkutano huo mjini Mombasa ambao  baada ya hapo waliendelea na mkutano wao katika mji wa Nakuru huku wakiwa na idadi kubwa ya wafuasi.

Wakongwe hao wa siasa walitangaza kuungana wiki iliyopita ambapo walisema lengo lao ni kujenga umoja wenye nguvu kiasa.

Wanasiasa hao walipata umati mkubwa wa wafuasi ambao wengi wao ni kutoka chama cha  TNA huku wengine wakitokea chama cha URP.

Wakiwa katika uwanja wa Afra waliweza kuelezea malengo yao ya ambapo walisema kubwa kwa ni kujenga umoja pamoja na kukuza demokrasia ya nchi hiyo.

Nyumba nyingi za wageni zikiwemo hoteli zilikuwa zimejaa watu siku ya Ijumaa katika mji wa Nakuru, ambapo wafuasi wa wanasiasa hao walimiminika kutokea maeneo mbalimbali kusikia maneno ya wanasiasa hao.

Wafuasi hao wengi wao walikuwa wakitokea  maeneo ya Rift Valley,  pembezoni mwa   na  Nairobi walianza kuingia Nakuru Jioni kushuhudia muungano huo wa viongozi wao wa vyama vya TNA na URP.

Mgombea wa Urais kwa mujibu wa makubaliano yao ni Uhuru Kenyatta huku  Williamu Ruto akitarajiwa kuwa Makamu wake.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger