Kikwete awataka wanasiasa wasiwatetee wavamizi wa misitu - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Kikwete awataka wanasiasa wasiwatetee wavamizi wa misitu

Kikwete awataka wanasiasa wasiwatetee wavamizi wa misitu

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, January 10, 2013 | 11:07 PM

RAIS Jakaya Kikwete  





Kwa ufupi


Alisema baadhi ya wanasiasa wanadiriki hata kuwatetea wananchi wanaovunja kwa makusudi sheria za nchi, wakati wakijua kuwa wanahatarisha masilahi ya wengi.

RAIS Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa nchini kusema ukweli katika mambo yenye masilahi kwa taifa badala ya kuzungumza uwongo kwa lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa.


Rais Kikwete aliyasema hayo jana, alipokuwa akizindua Mradi wa Maji katika Bwawa la Igombe mkoani Tabora.

Alisema baadhi ya wanasiasa wanadiriki hata kuwatetea wananchi wanaovunja kwa makusudi sheria za nchi, wakati wakijua kuwa wanahatarisha masilahi ya wengi.
Alisema katika baadhi ya maeneo, wananchi wamediriki kuvamia hifadhi za misitu na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira, lakini baadhi ya wanasiasa, wanawakinga kifua.

Hata hivyo Rais Kikwete aliwataka viongozi na watendaji kuwachukulia hatua za kisheria wananchi wa aina hiyo kwa kuzingatia kuwa vitendo vyao vinaathiri utunzaji wa vyanzo vya maji.

Alisema Mkoa wa Tabora ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na tatizo la uhaba wa maji, unaotokana na uharibifu wa vyanzo vya maji.

Alisema viongozi wakisimama kitede katika kulinda mazingira na kutoa elimu kwa wananchi, athari za ukataji miti na uharibifu wa mazingira, zitapungua na hivyo kuviwezesha vyanzo kubaki katika hali ya usalama.

Aliwataka viongozi wa Serikali wasione aibu kulinda misitu ya Serikali pale wanapoona kuwa imevamiwa na wananchi na kuendesha shughuli za kibinadamu.

Alisema mito mingi imekauka kwa sababu ya kuvamiwa na watu na kuendesha shughuli hizo.
Wakati huohuo, Rais Kikwete jana aliweka jiwe la msingi la Uwanja wa Ndege unaoendelea kujengwa mkoani Tabora, ambao utagharimu Sh11 bilioni, utakapokamilika.

Alisema Serikali ikikamilisha miradi ya ujenzi wa barabara katika Mkoa wa Tabora kwa kiwango cha lami na uwanja huo wa ndege, itakuwa imeufungua mkoa huo katika ukuzaji wa kiuchumi na kimaendeleo kwa wakazi wake.

Alisema Serikali imejipanga ili kukamilisha mradi huo ifikapo Machi mwaka huu.
Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe, alisema uwanja huo umejengwa kwa viwango vya kimataifa na kwamba utakapokamilika, utaruhusu ndege mbalimbali kuutumia .
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger