KLABU ya Real Madrid imekamilisha usajili wa kipa Diego Lopez kutoka klabu ya Sevilla, zote za Hispania.
Mabingwa hao wa La Liga wamekuwa wakihaha kusaka kipa mwingine tangu kuumia kwa mlinda mlango wao namba moja, Iker Casillas katika mechi ya Kombe la Mfalme dhidi ya Valencia.
Huku Nahodha wao huyo akitakiwa kuwa nje ya Uwanja kwa wiki 12 baada ya kufanyiwa upasuaji jana mchana, Los Blancos haijapoteza muda kumnasa mkongwe mwenye umri wa miaka 31, Lopez, ambaye alijiunga na klabu hiyo akiwa kinda.
Taarifa kutoka tovuti ya klabu hiyo imesema: "Real Madrid C.F. na Sevilla F.C. zimefikia makubaliano ya uhamisho wa Diego Lopez, ambaye atakaa katika klabu hadi mwishoni mwa msimu wa 2016/17."
Awali, Real Madrid ilihusishwa na mpango wa kumchukua kipa wa Bayer Leverkusen, Rene Adler azibe pengo la Casillas.
Lopez sasa atachuana na Antonio Adan kuwania namba kuelekea mchezo na Getafe mwishoni mwa wiki hii.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !