UKuta wajeruhi na kuharibu magari stendi ya Ubungo Dar - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » UKuta wajeruhi na kuharibu magari stendi ya Ubungo Dar

UKuta wajeruhi na kuharibu magari stendi ya Ubungo Dar

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, January 21, 2013 | 1:16 AM

Magari yaliyoharibiwa baada ya ukuta kuanguka stendi ya Ubungo jijini Dar es Salaam

Mpango wa Ujenzi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam leo umesababisha hasara kubwa kufuatia kuanguka kwa ukuta wa ndani kwenye maegesho  ya magari madogo.

Kwa mujibu wa taarifa ya mpita njia wa ameeleza kuwa baada ya ukuta huo kuanguka magari pamoja na  baadhi ya watu wameweza kujeruhiwa, hata hivyo jitihada za makusudi za kupunguza uharibifu zinaendelea.

"nipo hapa tokea alfajiri nilikuwa namsindikiza mgeni wa ndugu yangu, ghafla nikasikia kishindo kikubwa kutahamaki watu wakaanza kukimbilia eneo la tukio nilipofika hapa nikakuta kumbe ukuta huu eneo la maegesho ya magari madogo umebomoka.

Aidha taarifa za awali zimeeleza kuwa huenda kukawa na watu waliokufa kwani baadhi ya watu hupenda kukaa katika eneo hilo wakisubiri kufanyika kwa biashara mbalmbali.Ingawa pia zimeeleza kuwa majeruhi wa tukio hilo wamekimbizwa katika kituo cha afya cha Palestina kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Aidha watu wamehoji kwa nini wahusika wa ujenzi huo waanze kuvunja kuta hizo alfajiri wakati wanajua kuwa kunakuwa na pilikapilika nyingi, pamoja na hayo jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa suala hilo.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger