Maji yakiwa yamezingira nyumba mkoani Mtwara baada ya mvua kubwa kunyesha |
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imenyesha leo majira ya asubuhi mkoani Mtwara na kusababisha mafuriko huku ikiwaacha watu wengi kukosa makazi.
Mvua hiyo inayodaiwa kunyesha kwa masaa manne imehatarisha maisha ya wananchi mkoani humo kufuatia kuharibu barabara, nyumba mazao na maeneo mengine ya biashara jambo linaloelezwa na wakazi wa eneo hilo kuwa imeongeza ugumu wa maisha.
Pamoja na kasi ya mvua hiyo iliyosababisha kujaa kwa maji katika maeneo mengi, taarifa za vifo bado hazijaelezwa ingawa wananchi wameomba msaada wa hali na mali kutoka kwa serikali ili kunusuru maisha yao katika kipindi hiki.

0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !