BARAZA la Madiwani wa Halmahsauri ya Wilaya ya Arusha lilokaa jana tarehe 5,Januari.2013 limeidhinisha kuliachia eneo la Lakilaki lililopangwa kujengwa mji wa mfano wa Arusha (Arusha Safari Town) na kukabidhi hati miliki ya ardhi hiyo, kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Taasisi za umoja ya Mataifa na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Maamuzi hayo, yalifikiwa e katika kikao cha dharura ambacho, kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Hawa Ghasia, baada ya serikali kukubali kulipa mkopo uliokopwa na Halmashauri hiyo, Benki ya biashara ya Afrika (CBA) kiasi cha sh 8.6 bilioni pamoja na riba sambamba na kurejesha gharama za mradi huo kiasi cha sh 788.2 milioni na faida ambayo Halmashauri hiyo, ingepata kiasi cha sh5.6 bilioni.
Akizungumza mara baada ya Madiwani hao, kwa kauli moja kukubali kulitoa eneo hilo, Waziri Ghasia alisema Serikali imekubali kulipa gharama hizo, ili kuhakikisha inapatikana ardhi hiyo kwa manufaa ya Taifa zima.
“ndugu zangu kabla ya leo kuja hapa, tulikuwa katika kikao cha kutafuta muafaka wa jambo hilo ambacho kiliongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi na watendaji toka ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali, Wizara ya Ardhi Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa”alisema Waziri Ghasia.
Waziri huyo, pia alisema Rais Jakaya Kikwete alikuwa akifuatilia kupatikana kwa ardhi hiyo na ameiondoa hofu halmashauri hiyo, kupoteza fedha ambazo tayari wametumia na ambazo wangepata kama wangetekeleza mradi huo.
Hata hivyo, kabla ya madiwani hao, kukubali kutoa ardhi hiyo, walitaka uthibitsho wa maandishi wa Serikali kukubali kulipa deni la benki na gharama zote, hoja ambayo ilikubaliwa na waziri huyo, ambaye alisema tayari aliandika barua kwa halmashauri hiyo kueleza jinsi watakavyorejeshewa fedha zao.
“jamani mimi ni mtu mzima siwezi kuja hapa kusema ahadi ambazo hazipo,ninawahakikishia mtalipwa na mimi tayari niliandika barua kuelezea jambo hili naomba muiamini serikali yenu ahadi hii sio yangu ni ya serikali”alisema Waziri Ghasia.
Awali mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha, Halfani Hida alisema mradi wa awali kama ungetekelezwa tayari walikuwa wamepima jumla ya viwanja 348 ambavyo vingegawanywa kwa wananchi na kuipatia halmashauri hiyo mapato ya sh 13.3 bilioni, pia viwanja vya biashara biashara vingeingiza mapato ya sh 1.7 bilioni huku maeneo ya huduma yalitarajiwa kuingiza sh 332.6 milioni.
“baada ya mauzo ya viwanja tungepata sh 15.5 bilioni na hivyo baada ya kutoa gharama mbali mbali ikiwepo mkopo wa bemki ,halmashauri ingepata kiasi cha sh 4.9 bilioni”alisema Hida.
Eneo hilo la laki laki lina ukubwa wa ekari, 430 lilinunuliwa na halmashauri hiyo toka kwa Valahala Estate limited kwa sh 8.6 bilioni lakini wakati mradi ulipotaka kuanza ndipo mgogoro uliibuka baina ya halmashauri na watendaji wa serikali nje ya halmashauri na ndipo baadaye eneo hilo lilitwaliwa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi ambao ili kuchukuliwa na Wizara ya Mambo ya Nje.

0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !