KIBO PALACE HOTELI RAFIKI WA MAZINGIRA JIJI LA ARUSHA - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » KIBO PALACE HOTELI RAFIKI WA MAZINGIRA JIJI LA ARUSHA

KIBO PALACE HOTELI RAFIKI WA MAZINGIRA JIJI LA ARUSHA

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Saturday, January 5, 2013 | 6:52 PM

Written by 
Mkurugenzi Mkuu wa Palace Hoteli Arusha, Fred Maina akizungumza na Mwandishi wa Habarimpya.com,hayupo pichani        Arusha
JIJI la Arusha imefanikiwa katika suala la Utalii na Uwekezaji huku ikikabiliwa na Changamoto za usafi . Jiji hilo limeweza kupiga hatua zaidi na kutambulika vyema Afrika Mashariki na Kati lakini mamlaka zinazohusika zimeshindwa kutatua changamoto za usafi.
Katika sekta ya uwekezaji jiji la Arusha linapambwa na hoteli nyingi zenye hadhi ya nyota tano na moja ya Hoteli nzuri na za kisasa ni Palence Hoteli Arusha iliyopiga hatua kubwa katika kipindi cha miezi 11 tangu kuanzishwa kwake.
Watu mbalimbali wakiwa wamepumzika katika bustani ya Jiji la Arusha inayotunzwa na Palace Hoteli Arusha.Akizungumza na Habarimpya.com hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli hiyo Fred Maina anasema kwamba mbali na kuzingatia ubora wa vyakula, malazi huduma nzuri kwa wageni pia wamefanikiwa katika suala la kuhifadhi mazingira baada ya kutengeneza miundombinu mizuri ya maji taka na kuboresha mazingira ya nje ya Hoteli.
“Tumeamua kuiboresha bustani iliyoko mbele ya Hoteli yetu na kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Jiji la Arusha eneo hilo limekuwa kivutio kikubwa kwa waandaaji wa sherehe ya kipaimara, harusi kuja kupiga picha za kumbukumbu nani sehemu nzuri ya kupumzikia nyakati za mchana na usiku”anasema Maina.

Hii ndiyo maegesho ya magari yanayolindwa wa Askari wa Palace Hoteli Arusha.Picha zote na Jackson OdoyoMbali na Bustani hiyo,Palace Hoteli imefanya maboresho makubwa ya maegesho ya magari katika eneo la bustani hiyo yenye ulinzi na usalama wakutosha.
Palace Hoteli Arushai iko katikati ya Jiji, inamalengo makubwa ya kuhakikisha wageni wote wanaofika katika Jiji hilo kwa shuguli mbalimbali za kikazi,biashara na mikutano wanapata huduma safi ya malazi na vyakula kwa bei nafuu.
Hoteli hiyo iko karibu na Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (AICC),Makao Makuu ya Afrika ya Mashariki na Kati,(EAC).
Wakati Palace Hoteli Arusha ikijivuna kuwa rafiki wa mazingira, jijini  Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dk. Terezya Huvisa mwaka jana mwishoni aliifunga Hotel ya Double Tree kwa kushindwa kutunza mazingira.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger