AU yatuhumu ICC kwa kuandama Afrika - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » AU yatuhumu ICC kwa kuandama Afrika

AU yatuhumu ICC kwa kuandama Afrika

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, May 27, 2013 | 1:50 PM

Uhuru Kenyatta alichaguliwa kama rais wa nne wa Kenya mwezi Machi

Muungano wa Afrika umeituhumu mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kuwaandama wafrika kwa sababu ya rangi yao.

AU inapinga hatua ya ICC kusisitiza kusikiliza kesi za washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu.

Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn aliyasema hayo akiongeza kuwa italalamika mbele ya Umoja wa Mataifa kuhusu hilo.

Rais Kenyatta anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Julai kusikiliza mashtaka dhidi yake kuhusu uhalifu dhidi ya binadamu.

Aidha Kenyatta amekanusha tuhuma hiuzo ambazo zinatokana na madai ya kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007 ambapo maelfu walipoteza maisha yao na wengine kuachwa bila makao.

Alichaguliwa kama Rais katika uchaguzi uliofanyika mwezi Machi na kumshinda mpinzani wake mkubwa Raila Odinga katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali.

Akihutubia kikao cha marais wa Afrika kwenye mkutano wa AU mjini Addis Ababa , bwana Hailemariam alisema kuwa viongozi wa Afrika wameelezea wasiwasi kuwa asilimia 99 ya wale wanaotakikana na mahakama ya ICC kwa makosa yoyote yale ni waafrika.

"hii ni dalili ya kuwa mambo sio sawa, mfumo wa ICC una hujuma,'' alisema bwana Hailemariam
Mahakama ya ICC ilibuniwa ili kuangamiza kile kilichoonekana kuwa viongozi wanaofanya uhalifu bila kujali, lakini sasa ''mfumo huo umegeuka na kuwa mfumo wa kuwaandamana watu kwa misingi ya rangi,'' alisema bwana Hailemariam.

''Mahakama ingali inawataka Kenyatta na Ruto licha ya jamii zao zilizokuwa na uhasama katika uchaguzi wa 2007 kuungana na kuwachagua wawili hao kuwa viongozi wa Kenya,'' aliongeza bwana Hailemariam.

Bwana Kenyatta na Bwana Ruto walikuwa wapinzani wakuu katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2007 ambo ulifuatwa na mauaji ya watu 1,000 na wengine laki sita kuachwa bila makao.

Wadadisi wanasema kuwa kesi za ICC ziliwapatanisha wawili hao kushikrikiana katika uchaguzi wa 2013, kwani waliamini kuwa jamii ya kimataifa ilikuwa inaingilia maswala ya ndani ya Kenya
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger