Na Mashaka Mhando,Korogwe
WILAYA ya Korogwe mkoani Tanga, imetia fora katika mbio za Mwenge wa Uhuru uliomaliza mbio zake mkoani hapa jana, kwa kuwapanga wananchi kuulaki mwenge huo kila ulipokuwa ukipita katika vijiji mbalimbali.
Mwenge huo uliopokelewa katika Kijiji cha Makole kilichopo kata ya Magamba-Kwalukonge kutokea wilaya ya Kilindi, Mkuu wa wilaya hiyo Mrisho Gambo mara baada ya kuupokea mwenge huo, alisema kwamba utakimbizwa na kufungua miradi saba yenye jumla ya sh. 1,392,142,300.
Akizungumza katika mikutano mbalimbali katika kutoa ujumbe wa mwenge mwaka huu, kiongozi wa mwenge huo Juma Ali Simai, alirejea kauli yake ya kuwataka Watanzania kuepuka migogoro inayoweza kuwagawa na kuvunjika kwa amani.
Alisema baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alitumia baiskeli wakati akihamasisha wananchi kudai uhuru na maara baada ya kupata alijenga misingi ya umoja, mshikamano na upendo miongoni mwa Watanzania.
Hivyo, watu wanaochezea amani kwa kutaka kuwagawa wanafanya makosa makubwa ni vema wananchi wakaacha kuwaunga mkono kwani wapo wananchi wan chi nyingine wamekuwa hawatembei nyakati za mchana na usiku kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
“Wapo wenzetu wengine katika nchi zao hawatembei kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe, hawa wanajiuliza hivi Tanzania wamefanya nini hadi leo wana amani…Jamani hii amani tuilinde tuache kubaguana kwa misingi ya dini, rasilimali tuendeleze mshikamano tuliokuwa nao,” alisema Simai.
Akizungumza katika mkesha wa mwenge katika kijiji cha Kwashemshi, mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani ‘almaarufu Profesa Majimarefu’, alisema wilaya hiyo bado imekuwa na mshikamano miongoni mwa wananchi kiasi kwamba, wanatumia nafasi hiyo kufanya kazi za maendeleo katika vijiji vyao.
Mkesha huo uliombatana na watu kupima VVU na Ukimwi pamoja na watu mbalimbali kujitokeza kutoa damu kwa hiari katika zoezi ambalo pia Mwandishi wa habari hizi Bw. Mashaka Mhando, alitoa damu kiasi cya unit moja kati ya unit 50 zilizopatikana.
Mhando alisema ameaamua kutoa damu kwasababu wilaya ya Korogwe katika hospitali ya magunga huwa majeruhi wengi wamekuwa wakipata shida kubwa ya kuongezewa damu hivyo uhamasishaji wao wa kutoa damu salama unatakiwa kuungwa mkono.
Mwenge umamaliza mbio zake mkoani Tanga na leo umeanza mbio zake mkoani Kilimanjaro kwa kuanzia wilaya ya Same.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !