Hali nchini Syria inaendelea kuwa mbaya kila kukicha |
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza William Hague amesema kuwa vikwazo vya silaha ambavyo Muungano wa ulaya uliiwekea Syria vimeondolewa .
Akizungumza baada ya mkutano wa siku moja na mawaziri wengine wa mambo ya nje wa muungano wa Ulaya mjini Brassels, Bwana Hague alisema kuwa hakuna uamuzi wa moja kwa moja wa kutuma silaha kwa waasi wa Syria , na kwamba vikwazo vingine vitaendelea
Ni dhahiri kuwa uamuzi huo hautafanya mabadiliko makubwa mashinani kwa muda wa hivi karibuni. Hakuna hatua itakayochukuliwa hadi Agosti. Hapo ndipo Jumuiya ya Ulaya itakapochunguza upya hali ilivyo nchini Syria.
Inatarajiwa kuwa wakati huo Uingereza, Ufaransa na mataifa mengine yanayotaka kuchangia silaha kwa waasi wataruhusiwa kufanya hivyo.
Uamuzi huo utategemea mkutano mkubwa wa kibalozi utakaofanywa kati ya Marekani na Urusi mwezi ujao. Hata hivyo mkutano huo hauna uhakika wa kufanyika kwa sababu muungano wa makundi ya upinzani nchini Syria haujakubaliana kama wahudhurie au wasihudhuria mkutano huo licha ya utawala ya Rais Assad kusema kuwa unakubaliana na mkutano huo.
Mwandalizi mkuu wa mkutano huo, ambaye ni Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uingereza William Hague amesema kuwa tamko la Serikali ya Rais Assad kuwa huenda ukahudhuria mkutano huo ni la kutia moyo.
Ishara zote kutoka mashinani hadi sasa ni kuwa itachukua muda mrefu kabla ya wananchi wa kawaida kukubaliana na mapendekezo yanayotolewa na Jumuiya ya Ulaya.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !