Mtuhumiwa anayedaiwa
kumgonga na kumuua askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Koplo
Elikiza Nnko,
Jackson Simbo akipandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni
jijini Dar es Salaam.
Picha na Michael Jamson
|
Dereva Jackson Simbo (43), amefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kinondoni, kujibu shtaka la kusababisha kifo cha askari wa Kikosi
cha Polisi cha Usalama Barabarani, Elikiza
Nnko.
Mshtakiwa huyo, alifikishwa mahakamani jana.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ladislous Komanya, alidai kuwa mshtakiwa alitenda
makosa hayo Machi 18 mwaka huu, katika
eneo la Bamaga, Barabara ya Bagamoyo.
Wakili Komanya alidai kuwa
pamoja na shtaka hilo,
mshtakiwa pia anakabiliwa na shtaka la
kuingilia msafara wa kiongozi, kinyume na sheria. Wakili alidai kuwa akiwa
katika sehemu hiyo ya Bamaga,
mshtakiwa aliingilia msafara wa kiongozi
na kushindwa kuheshimu maelekezo yaliyokuwa yakitolewa kwa ishara na askari
huyo.
Komanya aliendelea
kudai, Simbo pia anakabiliwa na shtaka la
shindwa kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi hadi alipo
tafutwa na vyombo vya dola.
Hata Hivyo kwa upande wake, mshtakiwa alikana tuhuma dhidi
yake na Hakimu Kwey Lusemwa aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 15, mwaka huu.
Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana baada ya wakili wake
Edward Chuwa, kuomba mteja wake adhaminiwe kwa kuwa ametimiza masharti ya dhamana.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !