Mbunge Rose Kamili Sukum
|
Na Mussa Juma
Arusha.Polisi Mkoa wa Manyara inamsaka Mbunge wa Viti wa
Mkoa wa Manyara(Chadema ),Rose Kamili pamoja na watu wengine wanne kwa tuhuma
za kufunga ofisi ya kijiji cha Basotu kwa zaidi ya wiki moja sasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa alisema
jana kuwa wanamsaka mbunge huyo,pamoja na wenzake ili watowe maelezo kuhusiana
na tukio hilo kabla ya kufikishwa mahakamana.
Mbunge Kamili alipoulizwa jana kuhusiana na kusakwa huko,
alikiri kupata taarifa lakini akasema,kama polisi wanamuhitaji wamfuate
nyumbani kwani wanapajua.
Hata hivyo, alisema uamuzi wa kufungwa ofisi hiyo,
yalitolewa kwenye mkutano wa mkuu wa kijiji,kutokana na kupinga unyanyasaji wa
viongozi wa kijiji, kutosoma mapato na matumizi tangu mwaka 2007 na pia
kuwataka wafike Basotu viongozi wa wilaya.
Wananchi 365 walioshiriki mkutano mkuu huo wa kijiji, licha
ya kufunga ofisi hiyo pia walichagua vijana waliopitia mafunzo ya mgambo
kulinda ofisi hizo hadi muafaka utakapopatikana.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !