Mwenyekiti wa bodi ya
mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingiara mjini Moshi ,Shally
Raymond akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni.
|
Mkurugenzi wa manispaa ya
Moshi Bernrdette Kinabo akiotesha mti katika chanzo cha maji wakati wa kilele
cha maadhimisho ya wiki ya maji iliyofanyika katika kata ya Kaloleni.
|
Kaimu mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro Dk Ibrahim Msengi akiotesha mti katika chanzo cha maji cha kaloleni
wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji iliyofanyika katika kata hiyo.
|
Bomba linalotoa maji
katika kisima cha kaloleni na hatimaye kuunganishwa katika mtandao wa maji kwa
ajili ya wakazi wa Mabogini,Pasua na Bomambuzi.
|
HALMASHAURI ya Manispaa
ya Moshi imewatoa hofu wakazi wa kata za Kaloleni, Pasua na Mabogini wanaotumia
maji kutoka kisima cha Kaloleni kwamba
ni salama kwa matumizi ya nyumbani licha ya taarifa kuwa yanaathiriwa na dampo
lililopo jirani.
Wakizungumza katika
kilele cha wiki ya maji,mkurugenzi wa manispaa,Bernadette Kinabo na kaimu
mkurugenzi wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Moshi (MUWSA),Isa Osena
wamesema kisima hicho ni kirefu na hupimwa kitaalamu kila mwezi.
Kauli hiyo ilifuatia
kitendo cha wananchi wa kata hiyo,kumpokea kwa mabango yenye ujumbe
mbalimbali,kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dk Ibrahim Msengi wakilalamikia
usalama wa maji hayo lakini pia kutopata maji licha ya kisima kuwapo kwao.
Mwenyekiti wa mtaa wa
Kaloleni,Ndama Bin Ndama,alisema wananchi hawana imani na maji hayo kutokana na
majitaka yanayochurizika kutoka katika dampo kuu,lakini pia hawana maji licha
ya kuwepo kisima eneo lao huku wakilalamikia maji kupelekwa kata za jirani.
Katika majibu yao,Kinabo
na Osena walisema kisima kina urefu wa mita 100 na hupimwa kila mara na dampo
likiwa umbali wa zaidi ya mita 60 na limetengenezwa kitaalamu kwa kuwekewa
msingi wa saruji inazozuia maji kuelekea katika kisima.
Aidha Kinabo alisema
MUWSA imetenga zaidi ya Sh Mil 236 kwa mwaka wa fedha 2013/204 kwa ajili ya
kuongeza vyanzo vipya huku manispaa ikitarajia kuzindua mpango wa uoteshaji
miti Mil 2 katika vyanzo na makazi kuanzia April 10 hadi 16 mwaka huu.
Awali kaimu mkuu wa
mkoa,Dk Msengi akizindua kisima cha Kaloleni kilichoongeza uzalishaji wake
kutoka lita za ujazo 71 kwa saa hadi lita 1200 kwa siku na kukarabatiwa kwa Mil
41.2, alitaka wananchi
kukilinda na kuotesha
miti kwa wingi.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,Moshi
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !