JENGO LA GHORAFA 16 LADONDOKA DAR ES SAALAM LEO - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » JENGO LA GHORAFA 16 LADONDOKA DAR ES SAALAM LEO

JENGO LA GHORAFA 16 LADONDOKA DAR ES SAALAM LEO

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Friday, March 29, 2013 | 7:41 AM

jengo
jeng1
jeng2


Vijana walikuwa wakicheza mpira jirani na jengo hilo nao walijeruhiwa vibaya

jengo3


Magari yalifukiwa na kuharibika vibaya


TAARIFA YA UHAKIKIKA KABISA ILIYOIFIKIA GLOBU YA Arusha Forum HIVI PUNDE INAELEZA KUWA JENGO MOJA LA GHOROFA 16 LILIPO JIRANI NA MSIKITI WA SHIA ULIOPITA KATIKA MTAA WA IDRA GHAND,KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM,LIMEPOROMOKA MUDA MFUPI ULIOPITA

INAELEZWA KUWA MPAKA SASA WATU 17 WAMEOKOLEWA HUKU WAWILI WAKIWA WAMEPOTEZA MAISHA,NA JUHUDI ZA ZIADA ZINAENDELEA KUFANYWA ILI KUOKOA WENGINE WENGI WALIOFUKIWA NA KIFUSI HICHO.

MKUU WA MKOA WA JIJI LA DAR ES SALAAM,MH. SAID MECK SADICK PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE MBALIMBALI WAPO ENEO LA TUKIO HIVI SASA AKISHIRIKIANA NA WADAU WENGINE WA VYOMBO MBALI MBALI VYA ULINZI NA USALAMA,KUHAKIKISHA UOKOAJI UNAFANYIKA KWA WAKATI. AIDHA UHABA WA VIFAA VYA UOKOAJI UNAWEZA KUCHELEWESHA ZOEZI HILO LA UOKOAJI. MINONGONI MWA VIFAA VINAVYOHITAJIKA HAPO NI PAMOJA NA MASHINE ZA KUPASULIA ZEGE, SCAVETA KWAAJILI YA UFUKUAJI.
 CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA JENGO HILO HAKIJAFAHAMIKA MPAKA SASA,KWANI KILA MTU YUPO KWENYE HEKAHEKA ZA UOKOAJI.
HATA HIVYO HABARI ZA NDANI ZINASEMA WATU 17 WAMEOKOLEWA NA WATU 2 WAMEKUTWA WAMEKUFA ILA BADO ZOEZI LA UHOKOAJI LINAENDELEA

PICHA NA VIDEO ZA TULIO HILO LA KUSIKITISHA ZITAWAJIA PUNDE TU,HIVYO TUVUTE SUBIRA KIDOGO. SOURCE: MICHUZI MEDIA
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger