Bavicha kwawaka moto, Shonza atimuliwa - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Bavicha kwawaka moto, Shonza atimuliwa

Bavicha kwawaka moto, Shonza atimuliwa

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Sunday, January 6, 2013 | 7:22 PM

Written by 
Mbowe             Dar es Salaam
MAKAMU Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) Juliana Shonza pamoja na baadhi ya wanachama wengine akiwemo Mtela Mwampamba, na  Habib Mchange wamefukuzwa uanachama katika chama hicho huku wengine wakisimamishwa uongozi na wengine kupewa onyo kali.
Hatua hii imetafsiriwa kuwa ni msimamo wa Dk Slaa pamoja na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ambao wameelezwa kuwa wanakisafisha chama kwa lengo la kuingia ikulu kwa kishindo mwaka 2015.
Kabla ya kutimuliwa Mwampamba aliwahi kugombea ubunge kupitia chadema katika jimbo la Mbozi wakati Mchange aligombea ubunge jimbo la Kibaha lakini kura hazikutosha.
Aliye pewa karipio kali ni Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Mbeya Mr Kasambala wakati Gwakisa anayetokea Wilayani Rungwe akisimamishwa uongozi wake.
Fuatana nasi kwa ajili ya habari zaidi

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger