Ndesamburo arejea na kusema yuko fiti kiafya - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Ndesamburo arejea na kusema yuko fiti kiafya

Ndesamburo arejea na kusema yuko fiti kiafya

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, January 24, 2013 | 1:22 PM

Kwa ufupi

“Ni kweli Ndesamburo amerejea Jumamosi na ndege ya Shirika la British Aiways na alitamka mwenyewe kuwa “Nimerejea na niko fiti,”alisema Lema akimkariri Ndesamburo.

MBUNGE wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema) 
MBUNGE wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema), amerejea nchini kutoka Uingereza alikokuwa akitibiwa na kusema sasa yuko fiti kuwatumikia wananchi wake.

Hata hivyo taarifa ya ujio wake ilifanywa kwa siri kiasi kwamba hata picha za kupokewa kwake Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) hazikuweza kupatikana.

Mbunge huyo anarejea nchini baada ya kukaa Uingereza tangu Septemba 2012.
Taarifa hizo zilithibitishwa na katibu wake, Basil Lema ambaye pia ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro.

“Ni kweli Ndesamburo amerejea Jumamosi na ndege ya Shirika la British Aiways na alitamka mwenyewe kuwa “Nimerejea na niko fiti,”alisema Lema akimkariri Ndesamburo.
Lema aliongeza kusema “Sasa mbunge wetu amerudi na ametangaza afya yake imetengemaa kikamilifu na yuko tayari kwa ajili ya kukuru-kakara za kuwatetea wananchi wake.”

Hata hivyo, jitihada za kumpata Ndesamburo kwa njia ya simu yake ya kiganjani jana zilishindikana kutokana na simu yake hiyo kuzimwa, lakini baadhi ya ndugu wa karibu walisema yuko fiti.

Novemba mwaka jana mwenyewe aliongea na gazeti hili na kuthibitisha kuwa anaumwa na anapatiwa matibabu nchini humo huku akiwatoa hofu wapiga kura wake kuwa hajazidiwa hata kidogo.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili juzi usiku, Ndesamburo alisema kwa sasa anaendelea vizuri na kwamba anasubiri ruhusa ya madaktari wake ili aweze kurejea nchini.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger