Mama amtaka Redds Miss Tanzania, Brigitte kujiheshimu - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Mama amtaka Redds Miss Tanzania, Brigitte kujiheshimu

Mama amtaka Redds Miss Tanzania, Brigitte kujiheshimu

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Saturday, January 12, 2013 | 10:42 PM

Mshindi wa Taji la Mis Tanzania 2012,Brigitte Alfred baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo. 
Kwa ufupi

"Miss Tanzania ni kioo cha jamii hivyo anatakiwa kujiheshimu na kulinda heshima yake kwani ni mmoja wa watu wanaotazamwa na Watanzania wote wakati wote."

 MAMA mzazi wa Miss Tanzania Brigitte Alfred, Verdiana Augustine amemtaka mwanaye kuepuka kashfa zinazoweza kuwaharibia sifa na maisha yake.

Verdiana alisema, kumekuwa na kashfa mbalimbali zinazowakumba washindi wa Miss Tanzania na kuyafanya mashindano hayo yaonekane ni yakihuni kitu ambacho si sahihi.

"Miss Tanzania ni kioo cha jamii hivyo anatakiwa kujiheshimu na kulinda heshima yake kwani ni mmoja wa watu wanaotazamwa na Watanzania wote wakati wote."

“Watu wengi wanachukulia Miss Tanzania ni ya kihuni, kitu ambacho siyo sahihi, hivyo washindi wanatakiwa kijiheshimu na kuhakikisha wanafikia malengo yao na kuepukana na kashfa ambazo zinaweza kuwaharibia  sifa,” alisema.

Naye Miss Brigitte alisema anachangamoto nyingi zinazomuandama, ikiwa pamoja na kufuta dhana ya kuonekana mashindano hayo si mazuri, kutokana na tabia zilizooneshwa na baadhi ya washiriki kwa siku za nyuma.

“Hii ni changamoto kubwa kwangu, sitaki kumtaja huyu au yule, lakini kuna warembo wengine wamechangia kuyafanya mashindano haya kupoteza hadhi yake.

“Mashindano ni mazuri na jamii inapaswa kuyaunga mkono, kwani inaleta changamoto nyingi katika maisha.
Naomba wazazi wazidi kuwaruhusu watoto wao kushiriki mashindano haya.”

Akizungumzia zawadi ya gari aliyokabidhiwa na  wadhamini wa shindano hilo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original, Brigitte alisema ilikuwa nzuri na ya kutia moyo mno.

“Wengi wa warembo wanaoshiriki ni wanafunzi wa vyuo au wametoka katika maisha ya kawaida ni vizuri akapewa gari atakaloweza kulimudu katika matunzo ya kila siku.

“Haileti maana kumpa gari ambalo kutengeneza tu ni sawa na kununua gari jingine. Mimi nafurahia zawadi yangu kwani gari ni zuri, lenye ubora na nalitumia hata na familia pamoja na shughuli zangu binafsi,” alisema.

Naye Meneja wa Redd’s Original, Victoria Kimaro alisema zawadi hiyo iliyotolewa ni bomba zaidi na wanaamini itaendelea kuboreshwa kila mwaka.

“Redd’s imedhamiria kumfanya mwanamke anayetwaa taji ajue thamani yake na kuweza kumudu maisha yake ya kila siku hata kwa kile tutakachompa, naamini tutaendelea na kufika mbali zaidi,” alisema Victoria Kimaro

 Mashindano yaa Redd's Miss Tanzania yalifikia hivi karibuni katika Ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam ambapo Brigitte aliyetwaa taji hilo na kukabidhiwa gari aina ya Noah pamoja na fedha taslimu sh 8milioni.

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger