Mwenyekiti AU amfagilia Kikwete kwa kusaka suluhu ya migogoro - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Mwenyekiti AU amfagilia Kikwete kwa kusaka suluhu ya migogoro

Mwenyekiti AU amfagilia Kikwete kwa kusaka suluhu ya migogoro

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Friday, January 18, 2013 | 11:40 AM

Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na mgeni wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Boni Yayi wa Benin baada ya viongozi hao kuzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ikulu Dar es Salaam .


RAIS wa Benin na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Dk Thomas Yayi Boni, amempongeza Rais Jakaya Kikwete na Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) kwa kutafuta suluhu ya migogoro ya kisiasa nchini Madagacsar na Mashariki ya DRC, bila kuchoka.

Rais Yayi Boni pia ameipongeza Tanzania kwa kuwa na uchumi unaokua kufikia asilimia saba na kusema kuwa mafanikio hayo si ya Watanzania pekee, bali ni ya Afrika nzima.

“Tunaona juhudi anazozionesha Rais Kikwete katika kutatua migogoro ya kisiasa Madagascar na Mashariki ya DRC, kupitia Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA) anayoiongoza kwa nafasi ya Mwenyekiti, kuna dalili nzuri za kufikia suluhu inayotakiwa hasa kwa Madagascar,” alisema.

Katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu, Dar es Salaam jana, Rais Boni aliyekuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, pia alimpongeza Rais Kikwete kwa kushughulikia suala la mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwa namna ya kidemokrasia.

Akizungumzia mgogoro unaoendelea nchini Mali, alisema AU imekubali kupeleka jeshi lake nchini humo, ili kudhibiti waasi.

Kwa upande wake, Rais Kikwete aliiomba SADC iipe ushirikiano Madagascar katika kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi na wakati wa uchaguzi kwa sababu imeonesha nia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioisumbua kwa muda sasa.

“Uamuzi wa kukubali kwa Rajoelina kutogombea Urais tena ni wa busara na wenye nia ya kumaliza matatizo ya kisiasa yaliyokuwepo. Nilipokutana naye mara zote alionesha nia ya kukubali pendekezo la SADC la kutogombea nafasi hiyo, lakini hakutaka itangazwe hadi atakapotangaza mwenyewe."

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger