UTPC YAKABIDHI VIFAA KWA VILABU VYA WANAHABARI MIKOANI - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » UTPC YAKABIDHI VIFAA KWA VILABU VYA WANAHABARI MIKOANI

UTPC YAKABIDHI VIFAA KWA VILABU VYA WANAHABARI MIKOANI

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Tuesday, January 22, 2013 | 2:30 PM


Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania umetoa vifaa vya kazi (vitendea kazi) vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 35 kwa kila klabu ya wanahabari Mikoani kwa lengo la kuboresha utendaji kazi, weledi na kujenga uchumi wa vilabu hivyo

Akikabidhi vifaa hivyo kwa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Lindi jana makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za Dar City Press Club,vifaa ambavyo ni pamoja na kamera, KOMPYUTA,Runinga na zana za kisasa za mikutano na semina (projector) Ikiwemo machine ya kopi(Photocopy) Makamu wa Rais wa UTPC Bi Jane Mihanji akimkabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa Lindi Press club,Abdulaziz Ahmeid amehimiza utunzaji wa zana hizo pamoja na nidhamu ya matumizi ili kukomboa waandishi Mikoani ikiwemo kujiongezea kipato..
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger