Mtoto ‘achomolewa’ shule, aozwa - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Mtoto ‘achomolewa’ shule, aozwa

Mtoto ‘achomolewa’ shule, aozwa

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Thursday, January 10, 2013 | 6:28 AM


Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Geita, Josephine Chagula.  

Kwa ufupi
Alisema msichana huyo aliyekuwa miongoni mwa watoto kumi waliokuwa wakigharimiwa na mbunge huyo katika masomo yao, ameozeshwa na  wazazi wake Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, msichana huyo alikuwa anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Lubungo.

 Mtoto anayesomeshwa na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Geita, Josephine Chagula ameachishwa masomo na kuozeshwa.

Taarifa  hiyo iliyomuumiza mbunge huyo, ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi  katika Wilaya ya Mbogwe, Julius Masubwa.

Masubwa ambaye pia ni Mbuge wa Bukombe alitoa maelezo hayo alipokuwa akizungumzia watoto wanaosomeshwa na mbunge huyo.

Alisema msichana huyo aliyekuwa miongoni mwa watoto kumi waliokuwa wakigharimiwa na mbunge huyo katika masomo yao, ameozeshwa na  wazazi wake Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, msichana huyo alikuwa anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Lubungo.

Alisema kwa kipindi kirefu alikuwa haudhurii masoma jambo lililoulazimisha uongozi kufuatialia na hatimaye kubaini kuwa ameozeshwa.

Ofisa Elimu ya Sekondari wilayani humo, Philbert Nyangahondi alisema alipata taarifa hizo lakini hana  uhakiki. Alisema hata hivyo atalifuatilia  na kwamba tatizo la utoro katika wilaya hiyo ni kubwa na kwamba linachangia na wazazi kutoona umuhimu wa kusomesha watoto.

Akikabidhi vifaa vya shule kwa ofisa elimu huyo Chagula alisema kitendo alichokifanya mzazi huyu ni cha kinyama na kuagiza mamlaka husika kuhakikisha kuwa mwanafunzi huyo anarudi shule ..mara moja na aliyemuoa, hatua za kisheria zichukuliwe.

“Natumia gharama zangu kuwasaidia watoto wa kike wanaoishi kwenye mazingira magumu lakini watu wanawaachisha shule, nimeumia sana  ofisa naomba suala hili lishughulikiwe haraka sana,” alisema Chagula.

Chagula anasomesha watoto 30 katika Mkoa wa Geita na katika Wilaya ya Mbongwe anasomesha watoto 10.

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger