UTULIVU WAREJEA MTWARA,ZAIDI YA 40 WAKAMATWA, PINDA NA NCHIMBI WATIA TIMU - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » UTULIVU WAREJEA MTWARA,ZAIDI YA 40 WAKAMATWA, PINDA NA NCHIMBI WATIA TIMU

UTULIVU WAREJEA MTWARA,ZAIDI YA 40 WAKAMATWA, PINDA NA NCHIMBI WATIA TIMU

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Monday, January 28, 2013 | 10:52 AM

Sehemu ya watuhumiwa wa vurugu za Mtwara wakikamatwa mmoja baada mwingine.
 Hali ya utulivu inadaiwa kurejea katika Wilaya ya Masasi mjini Mtwara baada ya vikosi vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Polisi kuungana kuweka ulinzi huku watu zaidi ya 40 wakiwa wamekamatwa kuhusika na matukio ya vurugu za jana.

Kutokana na vurugu hizo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi wako Mtwara wakiendelea na vikao vya kurejesha amani na utulivu mkoani hapo.

Pia inadaiwa mida ya asubuhi Jumapili,27,2013 jana palilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya vijana ambao walikuwa wamefunga barabara na kuwatoza ushuru batili wa Shilingi 5,000/= wenye magari kama sehemu ya kujipatia fedha kwa njia feki.
Aidha shughuli za ibada ziliendelea kwa utulivu zaidi.

Aidha vijana hao walivamia nyumba ya Anna Abdalah na kuiteketeza kwa moto, kabla ya kuivamia ofisi ya  CCM Wilaya na kuichoma moto pamoja na magari matatu inasemekana wamekwisha teketeza nyumba ya Mbunge wa Masasi (Mama Kasembe), Vifaa vya Mahakama ya Mwanzo pamoja na magari ya Halmashauri,Ofisi ya Elimu ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Vijini kabla ya kuchoma moto Ofisi ya Mali ya Asili.

Maandamano hayo yanasemekana yaliongozwa na Madereva wa bodaboda.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger