Home »
» Radi yaua mtalii Mlima Kilimanjaro
Radi yaua mtalii Mlima Kilimanjaro
Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Sunday, January 6, 2013 | 7:14 AM
Radi yaua mtalii Mlima Kilimanjaro
MTU mmoja raia wa Ireland, aliyefahamika kwa jina la Ian Mc Keever (42), amefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakati wakipanda Mlima Kilimanjaro.
Tukio hilo limetokea Januari 2 mwaka huu, saa 6:30 mchana
katika eneo la Kibao cha Moir Hut kwenye njia ya Londorosi.
Taarifa iliyotolewa jana na Meneja Uhusiano Hifadhi za Taifa, (TANAPA), Bw. Pascal Shelutete, alisema marehemu alifika
nchini kwa ajili ya kupanda mlima huo kama mtalii.
“Marehamu alikuwa na wenzake wakati akipanda mlima huu kupitia Kampuni ya Wakala wa Utalii ya Everlasting Tour Company Limited ya Mjini Arusha na walianza safari ya kupanda mlima Desemba 30,2012,” alisema Bw. Shelutete.
Aliongeza kuwa, baada ya kutokea ajali hiyo wageni wengine 21 waliokuwa pamoja na marehemu waliamua kuahirisha safari ya kupanda mlima huo.
Bw. Shelutete alisema kuwa watu wanne walionusurika katika ajali hiyo kwa sasa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa KCMC, iliyoko mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
“TANAPA kwa kushirikiana na kampuni hii tunaendelea na taratibu mbalimbali za kushughulikia suala hili na matibabu kwa watalii waliojeruhiwa,” alisema.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !