BARAKA KIBONA, MIAKA
30,MNDALI,MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILOLO AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO WA
BINADAMU HAPA AKIWA NDANI YA GARI YA POLISI
MTUHUMIWA AKIPAKIWA
NDANI YA GARI YA POLISI
HAYA MABOKSI
INNASADIKIWA YALITAKIWA YAJAE HELA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA
BAADHI YA WANANCHI WA MTAA WA ILOLO WAKISHANGAA TUKIO HILO NYUMBANI ALIKOPANGA MTUHUMIWA HUYO
MNAMO TAREHE
12.02.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO ENEO LA ILOLO JIJI NA MKOA WA MBEYA.
ASKARI POLISI WALIMKAMATA BARAKA S/O KIBONA,MIAKA 30,MNDALI,MFANYABIASHARA,
MKAZI WA ILOLO AKIWA NA KIUNGO CHA BINADAMU SEHEMU YA KIGANJA CHA MKONO WA
KULIA NDANI YA NYUMBA YAKE.
MBINU ILIYOTUMIKA NI
KUFICHA KIUNGO HICHO CHUMBANI NDANI YA BOX KWA KUZUNGUSHIWA KAMBA . MTUHUMIWA
ANAKIRI KUMILIKI KIUNGO HICHO AMBACHO ANADAI ALIPEWA NA MGANGA WAKE WA KIENYEJI
KWA MADHUMUNI YA KUKITUMIA KIUNGO HICHO KWA AJILI YA KUJIKINGA/KUJILINDA KATIKA
BIASHARA ZAKE ZA KIMACHINGA ZISICHUKULIWE KWA NJIA YA KISHIRIKINA IKIWA NI
PAMOJA
NA FEDHA ZAKE.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI
WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO JAMII KUACHA TABIA YA KUSADIKI IMANI ZA
KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WAFANYE KAZI ZAO KWA
BIDII KWA KUMCHA MWENYEZI MUNGU KUPITIA IMANI ZA DINI ZAO.
AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUENDELEA KUUCHUKIA
UHALIFU KWA KUWAFICHUA WAHALIFU NA UHALIFU KATIKA MAMLAKA HUSIKA UNAOJITOKEZA
KATIKA MAENEO YAO.
Signed by
[B.N.MASAKI -SSP]
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MBEYA
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !