Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Mhe.
Klaus-Peter Willsch, Kiongozi wa Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Bajeti ya Bunge
la Ujerumani alipokutana nae Wizarani kwa
mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania
na Ujerumani.
Mhe. Membe
akimsikiliza Mhe. Willsch wakati wa mazungumzo yao.
Mhe. Willsch (kulia
kwa Waziri Membe) akimsikiliza Mhe. Membe wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha
ni baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Ujerumani pamoja na Mhe.
Klaus-Peter Brandes ( wa sita kutoka kushoto), Balozi wa Ujerumani hapa nchini.
Wajumbe kutoka Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsilikiza Mhe. Membe (hayupo
pichani) wakati wa mazungumzo yake na Wabunge kutoka Ujerumani. Kutoka kushoto
ni Balozi Dora Msechu, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika,Bibi Zainab
Angovi, Afisa kutoka Idara ya Ulaya na Amerika na Bw. Grayson Ishengoma, Afisa
kutoka Idara ya Ulaya na Amerika.
Mhe. Membe akifurahia
Medali Maalum aliyokabidhiwa na Mhe. Willsch kama ishara ya kutambua
ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani.
Mhe. Membe akiwa
katika picha ya pamoja na Ujumbe huo.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !