Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za watu wenye
ulemavu wa ngozi nchini (Albino) Vicky Mketema kulia na wajumbe wenzake wa
shirika hilo
watatu waliosimama nyuma. Kulia waliosimama ni katibu wa Mkuu huyo wa Mkoa
Frank Mateni na kushoto aliyekaa ni Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa
Deonisya Njuyui.
Mama Maria Chambanenge mlemavu wa ngozi anayenyonyesha mtoto
wa miezi mitano alikatwa mkono na watuhumiwa ambao wameshatiwa nguvuni na jeshi
la polisi Mkoa wa Rukwa na Mkono wake uliokatwa umeshapatikana. Upelelezi bado
unaendelea kuwapata watuhumiwa zaidi wanaohusika na vitendo hivyo.
Mkurugenzi wa shirika la under the same sun Vicky Mketema
ametoa pongezi za dhati kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa kushughulikia tatizo
hilo kikamilifu na kwa haraka na kufanikiwa kupata kiungo hicho na watuhumiwa
waliohusika kwa muda wa siku mbili. Alisema endapo mikoa yote ingekuwa inashughulikia
matatizo kama hayo kwa muda mfupi kama huo
basi uhalifu na namna hii ungekuwa umeshatoweka nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ametoa onyo kali kwa
wale wote watakaohusika na vitendo vya uvunjifu wa amani Mkoani humo ambapo
amewataka wananchi kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya ulinzi pale wanapowashuku
wahalifu wa vitendo hivyo. Amewato hofu wananchi kwani vyombo vya ulinzi na
usalama vipo kwa ajili yo.
Muathirika huyo anaendelea kupata huduma za matibabu katika
Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na hali yake inaendelea vizuri.Picha Na Hamza
Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !