Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara (Mb) akisalimiana na Mkurugenzi wa British Council nchini Sally
Robinson (kulia) leo Ofisini kwa Waziri,alipokwenda kumtembelea na kufanya
mazungumzo mbalimbali kuhusu tasnia ya ubunifu wa Sanaa na Utamaduni pamoja na
jinsi ya kuwajengea uwezo katika fani mbalimbali za sanaa na ujasiria mali.
Waziri wa Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella
Mukangara (Mb) akizungumza na Mkurugenzi wa British Council nchini (kulia)
Sally Robinson leo alipomtembelea Ofisini kwake jijini
Dar es Salaam na
kuzungumzia masuala mbalimbali ya tasnia ya Utamaduni.
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo (kushoto)
Dkt. Fenella Mukangara akiangalia kipeperushi baada ya kupokea kutoka kwa
Mkurugenzi wa British Council nchini,Sally Robinson alipomtembelea leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote
na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !