NAIBU KATIBU MKUU WA UN
Na Mwandishi Maalum,
NEW YORK
Wakati viongozi wakuu
mbalimbali nchini Tanzania wakisisitiza haja na umuhimu wa viongozi wa
madhebu ya dini kuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara. Umoja wa Mataifa
nao kwa upande wake unaeleza kwamba ni
kwa njia ya mazungumzo
migogoro ya dini inaweza kuepukika.
Kauli hiyo ya Umoja
wa Mataifa, umetolewa na Jan Eliasson,Nabu Katibu Mkuu wa chombo hicho ya Kimataifa , wakati wa
tukio maalum la Muungano kwaajili ya utamaduni wa Amani kwa njia
ya maelewano ya madhehebu ya dini. Tukio ambalo limefanyika
mwishoni mwa wiki hapa umoja wa mataifa likiwahusisha wawakilishi kutoka dini mbalimbali, vyama visivyo vya kiserikali
na mabalozi.
“Migogoro mingi inayoendelea
hivi sasa duniani, ni migogoro ya
kidini. Mazungumzo baina ya imani mbalimbali yanaweza kusaidia kusuluhisha
migogoro hii. Tunaweza kupambana na
chuki kwa njia ya mazungumzo ili kujenga maelewano na kujenga daraja la maisha bora kwa jamii
zetu”.Akasema Naibu Katibu Mkuu
Na kuongeza kuwa, dini zote zimekuwa mstari wa mbele katika juhudi si tu za
kuhimiza amani na upendo, bali hata katika miradi ya kuwasaidia watu maskini kwa kutoa huduma kama vile za afya, na kuwasaidia vijana.
Hata hivyo akaonya
kwamba, siasa kali za kidini zimekuwa
chimbuko la uharibifu wa kudumu na
mateso katika jamii.
Na kwa sababu hiyo akasisitiza kutoachiwa kwa vikundi vya
dini vyenye misimamo mikali kuharibu na
kuvuruga amani na maendeleo na kazi
nzuri inayofanywa na madhehebu ya dini .
“Hatuwezi kuruhusu kundi dogo la watu wenye misimamo
mikali kuharibu kazi nzuri zinazofanywa
na jumuia za kidini kwa waumini wao
duniani kote” akahimiza Bw. Eliasson
Akaelezea wasi wasi
wake kuhusu vijana kutumiwa na vikundi
vyenye misimamo mikali kueneza kampeni
za chuki na vurugu kwa ahadi za kupata
dhawabu au wokovu ili wao watimize malengo yao.
“Kwa kawaida vijana
wana nguvu. Tunapashwa kutafuta
njia nzuri na sahihi za kuwafanya wazitumie nvugu zao kuboresha maisha yao” akasisitiza Naibu
Katibu Mkuu.
Naye Rais wa Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Vuk Jeremic kwa
upande wake alisema Umoja wa
Mataifa unaweza kufaidika sana kama viongozi wote wa dini watajihusisha na
kufanya kazi kwa moja ili kuleta amani. Huku akiutaka Umoja huo kuogeza kasi ya kushirikiana na
madhehebu ya dini.
“ Hebu basi na
turejee na kukumbatia wito unaotolewa na imani zetu, wito wa kuwasaidia watu
wengine wenye matatizo, wito wa kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe,ikiwa
ni pamoja na uhuru wa kuabudu
wakati wowote na mahali popote bila ya kujali tofauti zetu za imani”.
Rais huyo wa Baraza Kuu akasema kila mtu anawajibu wa
kuwasiliana na mwenzake na kusahau yaliyopitia na kuonya kwamba kama vyanzo
vilivyopita vya migogoro ya kidini
vitaendelea kukumbushiwa mara kwa mara, kuna hatari kubwa ya kuitumbukiza dunia
katika machafuko ya kutisha
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !