Obama ahimiza uchaguzi huru na wa haki Kenya - Arusha Forum
Headlines News :
Home » » Obama ahimiza uchaguzi huru na wa haki Kenya

Obama ahimiza uchaguzi huru na wa haki Kenya

Written By Sema Naye - Naipenda Tanzania on Tuesday, February 5, 2013 | 10:18 PM

RAIS Barack Obama
Kwa ufupi

“Zaidi ya yote, watu wa Kenya lazima muungane pamoja, kabla na baada ya uchaguzi, na kushirikiana kuijenga nchi yenu. Baada ya ghasia miaka mitano iliyopita, mumeshirikiana na kuijenga upya jamii, kufanyia mageuzi taasisi muhimu na kupitisha Katiba Mpya. Sasa Kenya lazima ichukue hatua nyingine mwezi Machi, kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya Katiba Mpya,” akasema.

RAIS Barack Obama wa Marekani amesema kuwa ingawa nchi yake haitaamua atakayechaguliwa kuwa rais wa Kenya, inafuatilia kwa karibu uchaguzi huo na kwamba, uamuzi wa Wakenya utaheshimiwa.

Kwenye hotuba maalumu aliyoitoa kupitia video kwenye mtandao wa YouTube jana, Rais Obama aliwahimiza Wakenya wawaepuke watu watakaowachochea au kutumia vitisho kushinikiza wachaguliwe.

“Kenya lazima iruhusu uchaguzi huru na wa haki. Wakenya waahidi kutatua mizozo ya uchaguzi mahakamani na wala si kwenye barabara,” alisema.
Maelezo haya yanafanana na yale aliyoyatoa zaidi ya miaka mitano iliyopita, wakati wafuasi wa chama cha ODM walipokataa matokeo ya uchaguzi wa urais na badala yake, wakaamua kuingia barabarani kudai ushindi baada ya kukosa imani na Idara ya Mahakama.

“Zaidi ya yote, watu wa Kenya lazima muungane pamoja, kabla na baada ya uchaguzi, na kushirikiana kuijenga nchi yenu. Baada ya ghasia miaka mitano iliyopita, mumeshirikiana na kuijenga upya jamii, kufanyia mageuzi taasisi muhimu na kupitisha Katiba Mpya. Sasa Kenya lazima ichukue hatua nyingine mwezi Machi, kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya Katiba Mpya,” akasema.

Rais Obama ambaye daima ameukumbusha ulimwengu kwamba asili yake ni Kenya, alianza kutoa ujumbe wake huo kwa salamu ya Kiswahili, “Habari yako” na kusema anakumbuka alivyopokelewa Kenya alipofanya ziara yake miaka kadhaa iliyopita alipokuwa Seneta wa jimbo la Illinois.


Alieleza kwamba uchaguzi ujao unaweza kuwa hatua muhimu ya kufikia demokrasia ya kweli, inayoongozwa na utawala unaoheshimu sheria na ulio na taasisi imara zinazotegemewa.

“Mkichukua njia hiyo na kukataa ghasia na kugawanyana, basi Kenya inaweza kupiga hatua na kutoa fursa kwa maelfu ya raia wake wenye vipawa, hasa vijana. Mkiendelea hivyo, mnaweza kuijenga Kenya yenye usawa, inayokataa ufisadi na inayoheshimu haki za wakenya wote,” alisema.

Alisema haoni njia bora ya kuadhimisha miaka 50 tangu Kenya ipate uhuru kuliko hii ya kufanya uchaguzi utakaokuwa huru na wa haki, hivyo kuwataka wanaopanga kushiriki katika azma ya kupata maendeleo kuwa marafiki wa kweli na Serikali ya Marekani.

Punde baada ya hotuba hiyo, Wakenya walieleza hisia zao kwenye mtandao.
David Kihugi alisema, “Sasa ndio ameona ukweli wa ghasia zilizotokea.”

Naye Ann Winjj alisema, “Tutawaambia kama watasikia kwa maana fujo ni mila yao.”

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Arusha Forum - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger