Hoyce Temu
akimsikiliza kwa makini Rais wa serikali
ya wanafunzi chuo
cha Tumaini Iringa
Hoyce Temu akipozi kwa picha na mzee wa matukio daima
Francis Godwin baada ya kufanya
mahojiano juu ya ziara yake mkoani
Iringa
Hoyce Temu
alipojichanganya vidanda vya UVCCM
na kukutana na wana, mwanahabari wa Chanel Ten Clement Sanga , Afande
Bashiri na mwanahabari Denis Mlowe
Wadau wakifurahi kuwa na mrembo Hoyce Temu
Miss Tanzania wa mwaka 1999
Hoyce Temu ametua mkoani Iringa na
kujichanganya na wananchi wakazi
wa mkoa wa Iringa katika maeneo
ambayo si rahisi kwa star kama
huyo kujichanganya .
Temu alishangaza
wengi na kuonekana ni mtu wa watu
baada ya kuacha kujirusha katika maeneo maarufu na kulazimika
kujichanganya na wana Iringa katika Grosari
za vibanda vya UVCCM mjini Iringa na kuwapa ofa ya
kinywaji wadau waliofika kumsabai kwa
salamu.
Hata hivyo Temu ambae
yupo mkoani Iringa kwa ajili ya
kuandaa kipindi chake cha MIMI
NA TANZANIA kinachorushwa
katika kituo cha Chanel Ten
amesema kuwa lengo lake ni kuendelea
kuheshimu taji lake kwa kufanya mambo
mazuri katika jamii badala ya
kujivunjia heshima yake .
Amesema kuwa
atapenda kuona watanzania wanaendelea kumpongeza kwa kazi zake badala
ya kuendelea kumdharau ,hivyo amesema ataendelea
kufanya makubwa katika Taifa.
Kwa upande wake
wakazi wa mkoa wa Iringa
walimpongeza mrembo huyo kwa kazi nzuri anazozifanya katika jamii na
kuwa katika maisha yake hapaswi kuiga mambo ya
warembo wengine ambao wameshindwa
kujiheshimu na kuonekana ni wachafu
wa kutupwa katika jamii kutokana na kuwa na skendo kila kukicha.
Bila kuwataja
majina ya warembo hao walisema kuwa picha ya kuwa urembo ni uhuni imekuwa
ikichafuliwa na warembo
wanaoshika nafasi kama hizo
na mara
baada ya kuwa maarufu wanaanza
kuutumia umaarufu huo kuuza miili
yao.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !