VIONGOZI waandamizi wa Chama Cha
Demokrasia
na Mendeleo CHADEMA pamoja na
wanachama 15 wa chama
hicho wanatarajia kujiunga na Chama Cha NCCR Mageuzi leo
katika ukumbi wa
Hotel ya Double J jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa taarifa za chama
hicho zilizotumwa kwa njia ya ujumbe
mfupi wa simu ya mkononi kwa wanahabari
imedaiwa
kuwa viongozi hao wa CHADEMA watakutana na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi na mshauri wa
mambo ya kisiasa Danda
Juju ambaye atamwakilisha, mwenyekiti wa Taifa
wa chama hicho
James Mbatia.Juju ambaye tayari amewasili mkoani
Mbeya kwa
shughuli hiyo maalum anatarajia kuwapokea viongozi hao wa
CHADEMA
ikiwa ni hatua za awali zinazodaiwa kukisambaratisha CHADEMA.
Hivi karibuni aliyewahi kuwa
Katibu wa Mkoa wa
CHADEMA Eddo Makata alitangaza
kujiunga na NCCR-Mageuzi
baada ya kujiuzulu kutoka
CHADEMA ambapo hata hivyo
viongozi wa CHADEMA
walidai kuwa walimtimua uongozi
na uanachama.
Wimbi la mpasuko ndani ya CHADEMA
limeanza kuibuka
baada ya madai ya kutimuliwa kwa viongozi
na wanachama wa chama
hicho akiwemo, Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana
la
Chadema Taifa (BAVICHA)Juliana
Shonza na aliyewahi kugombea
Ubunge jimbo la Mbozi Mashariki
Mtera Mwampamba
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !